Jumanne 18 Agosti 2026 - 12:45
Utawala vamizi unalenga kuidhalilisha Lebanon na kupiga pigo dhidi ya umoja wa kitaifa

Hawza/ Adui mhalifu wa Kizayuni anaendelea na uchokozi wake dhidi ya Lebanon, ardhi yake na watu wake, na ametenda mauaji mawili katika miji miwili ya Ansar na Deir al-Zahrani.

Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, adui mhalifu wa Kizayuni anaendelea na uchokozi wake dhidi ya Lebanon, ardhi yake na watu wake; hivi karibuni ametenda mauaji mawili dhidi ya raia wa kawaida wakiwa katika nyumba zao katika miji miwili ya Ansar na Deir al-Zahrani. Jambo hili linahitaji serikali kutathmini upya hesabu zake kuhusu mkondo inaoufuata wa kutoa masharti na upendeleo mbele ya matakwa ya kupindukia ya adui dhalimu.

Katika muktadha huu, Naibu Spika wa zamani wa Bunge la Lebanon, Elie Ferzli, katika mahojiano na tovuti ya habari ya “Al-Ahed”, snaamini kwamba; mvamizi analenga kuidhalilisha Lebanon, kuipiga pigo dhidi ya umoja wake na kutumia makubaliano yaliyopo ili kuimarisha hali mpya halisi.

Ferzli ametoa wito wa kutathmini upya namna ya kushughulikia kile kinachoitwa “Makubaliano ya Mfumo” na kutomruhusu Israel kuyatumia kama pazia la kuendeleza uchokozi wake, huku akisisitiza umuhimu wa kulinda umoja wa kitaifa.

Mpango wa Israel wa kuidhalilisha Lebanon

Ferzli anaamini kwamba; kinachotokea ni sehemu ya mpango wa Israel unaolenga kuidhalilisha Lebanon kwa ujumla, hususan makundi ambayo yamechagua kushirikiana na mkondo wa makubaliano na mazungumzo.

Alisisitiza: Mvamizi anafanya kazi ya kuchochea hali na kubashiri juu ya mwitikio wa watu ili kutumikia malengo yake ya kisiasa, hususan katika kivuli cha uchaguzi wa ndani wa Israel na jitihada za kutumia maendeleo ya kiusalama kwa ajili ya hesabu zake za kisiasa na uchaguzi.

Ferzli alieleza: Asili ya mpango huo imejitokeza wazi, na jambo hili linaifanya serikali ya Lebanon kuwajibika na katika kukabiliana nao kwa umakini zaidi na kutosheka na misimamo isiyoendana na ukubwa wa uchokozi na changamoto zilizopo.

“Makubaliano ya Mfumo” hayapaswi kuwa pazia la uvamizi

Ferzli alisisitiza kuwa: Kinachohitajika ni kutafuta nyenzo zitakazosaidia kuimarisha haki za Lebanon, badala ya kile kinachoitwa “Makubaliano ya Mfumo” kugeuzwa kuwa kifuniko cha kisiasa ambacho Israel itakitumia wakati ikiendelea na uchokozi wake dhidi ya Lebanon.

Kwa maoni yake, kuendelea na mazungumzo ya moja kwa moja katika hali hii kunaiweka Lebanon mbele ya mlinganyo usio na uwiano; kwa sababu haiwezekani kwa upande mmoja mchakato wa mazungumzo kuendelea, na kwa upande mwingine mvamizi akaendelea kutumia shinikizo la kijeshi na uchokozi.

Lebanon ilikuwa karibu kunufaika na makubaliano ya Iran; kwa nini serikali haikuendelea? Kisha Ferzli alizungumzia maendeleo yanayohusiana na mkondo wa Marekani na Iran, akiamini kwamba Lebanon ilikuwa mbele ya fursa ya kunufaika na makubaliano ya Iran.

Akieleza kwamba Lebanon ilikuwa karibu kunufaika na makubaliano hayo, aliuliza swali: Kwa nini serikali ya Lebanon haikuendelea kushirikiana nayo, maadamu jambo hilo halidhuru maslahi ya Lebanon?

Serikali inapaswa kulichukulia kwa uzito suala la ratiba ya kuondoka mvamizi

Ferzli alisisitiza: Serikali ilipaswa kung’ang’ania suala la muda uliowekwa, yaani ratiba ya kuondoka vikosi vya uvamizi, kwa sababu suala hili ni jambo la msingi katika kila mchakato unaolenga kushughulikia hali iliyopo.

Kwa maoni yake, kinachohitajika ni kuendesha mazungumzo kutoka katika msimamo unaolinda haki za Lebanon, wala si kutoka katika msimamo unaowaruhusu wengine kulazimisha masharti yao au kutumia makubaliano kufikia malengo yanayokinzana na maslahi ya Lebanon.

Ferzli anaamini kuwa: Kila mchakato wa kisiasa ambao hautapelekea katika kuimarishwa kwa haki za Lebanon na kusitishwa kwa uchokozi utabaki kuwa pungufu, hususan huku shinikizo la ardhini kutoka kwa mvamizi likiendelea.

Umoja wa kitaifa mbele ya mpango wa Israel

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Ferzli aliutoa ujumbe kwa wananchi wa Lebanon na makundi ya kisiasa, akiwataka kuendelea kuulinda umoja wa kitaifa mbele ya matukio yanayoendelea.

Akisisitiza kwamba kuhifadhi umoja wa ndani ni jambo la msingi katika kukabiliana na mpango wowote unaoilenga Lebanon, aliwataka kutoruhusu tofauti za kisiasa kugeuka kuwa lango la kudhoofisha hali ya ndani au kutumikia malengo ya mvamizi.

Mwisho wa hotuba yake, Ferzli alisisitiza jambo hili: Hatua ya sasa inahitaji msimamo mmoja wa Lebanon unaopanga upya vipaumbele na kuzuia makubaliano ya kisiasa yasigeuke kuwa nyenzo ambazo mvamizi ananufaika nazo, huku wakati huo huo ikifanya juhudi za kulinda haki za Lebanon na kuhifadhi umoja wa nchi.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha